الخميس، 27 ديسمبر 2018

BISHARA (MATUMAINI) 10 KWA WENYE KUDUMU NA KUSALI SALA YA ALFAJIRI KWA WAKATI:


BISHARA (MATUMAINI) 10 KWA WENYE KUDUMU NA KUSALI SALA YA ALFAJIRI KWA WAKATI:
___________________
✍🏾 Bishara ya kwanza:
 Amesema Mtume ﷺ: ((Wabashirie (wape matumaini) wanaotembe kwenye giza (la alfajri) kuelekea msikitini, (kwamba watapata) Nuru iliotimia siku ya Kiama))
رواه أبو داود والترمذي وصححه الألباني
---------------------------
✍🏾 Bishara ya Pili:
 Amesema Mtume ﷺ: ((Rakaa mbili za Alfajr ni bora kuliko Dunia (nzima) na vilivyomo ndani yake))
رواه مسلم
-------------------------
✍🏾 Bishara ya Tatu:
 Amesema Mtume ﷺ: ((Mwenye kutoka nyumbani kwake (kwao) kwenda msikitini (Alfajir) huandikiwa kwa kila hatua moja mema kumi, na mwenye kukaa msikitini anasubiri Sala ni kama mwenye kufanya Qunut, na huandikwa (yeye) katika wenye kusali mpaka arudi kwake))
أخرجه أحمد
----------------------------
✍🏾 Bishara ya Nne:
 Amesema Allah جل في علاه : ".....na kisomo cha (sala ya) Alfajir hakika kisomo cha (sala ya) Alfajr kimekua ni chenye kushuhudiwa (na Allah na malaika wake)"
الإسراء : ٧٨
--------------------------
✍🏾 Bishara ya Tano:
 Amesema Mtume ﷺ: ((Hatoingia Motoni yoyote ambae alisali (Alfajir) kabla ya kuchomoza Jua na (Alasiri) kabla ya kuzama Jua, inamaanisha Alfajiri na Alasiri"
رواه مسلم
-------------------------
✍🏾 Bishara ya Sita:
 Amesema Mtume ﷺ: (( Mwenye kusali Ishaa kwa Jamaa ni kama aliesimama (kusali) nusu (nzima) ya usiku, na mwenye kusali Subhi (Fajr) kwa jamaa ni kama aliesali Usiku mzima (kucha)
رواه مسلم
--------------------------
✍🏾 Bishara ya Nane:
 Amesema Mtume ﷺ (( Mwenye kusali Alfajr kisha akakaa katika msala wake (eneo lake la kuslia), malaika humsalia (sala ya malaika kwa mwanadam ni sala kilugha yani Dua) na sala yao kwake hua ni (hii) Ewe Allah msamehe, Ewe Allah Mhurumie))
رواه أحمد
-----------------------------
✍🏾 Bishara ya Tisa:
 Amesema Mtume ﷺ: (( Mwenye kusali mapema Alfajr kwa jamaa, kisha akakaa anamtaja Allah mpaka jua likachomoza (tu), kisha akasali rakaa mbili, anakua na ujira wa (mtu aliekwenda) Hajj na Umrah iliotimia iliotimia iliotimia))
رواه الترمذي وصححه الألباني
----------------------------
✍🏾 Bishara ya Kumi:
 Amesema Mtume ﷺ: (( Mwenye kusali sala ya Alfajr huyo yupo katika dhimma (dhamana) ya Allah, basi Allah hakuombeni kitu chochote (ili) kuingia katika dhamana yake....))
رواه مسلم
____________________
✍🏾 Twamuomba Alla atusahilishie kuisali Afajr kwa wakati na kwa jamaa kisha na sisi tupitishe juhudi zetu ili tuwe wadhaminiwa na Allah ni furaha ilioje kupata Sponsor ambae ni tajiri wa matajiri?

ليست هناك تعليقات:

إرسال تعليق