الجمعة، 10 أغسطس 2018

🌴NASAHA ZA ASUBUH🌴

تمت مشاركة ‏صورة‏ من قبل ‏‎Ikram Mohmmad‎‏.
IslamHouse.com Kiswahili - Swahili - سواحيلي
🌴NASAHA ZA ASUBUH🌴
Hajaj bin yusuf aliamrisha kukamatwa watu watatu kwa tuhuma fulani ,kisha wakatwe vichwa.
Walipofikishwa mbele ya mkata vichwa ...
Hajaj aliona kwa mbali mwanamke mrembo akilia 😭huku akijifuta machozi kwa kihengachifu..
Akasema hajaj: mleteni hapa .
Alipokwisha letwa , hajaji akamuliza:kipi kikulizacho?
Mwanamke akajibu:hao watu watatu ulioamrisha wakatwe vichwa vyao ni:mumewengu ,mwanangu na kaka yangu ,kwanini nisilie?
Hajaji kwa takrima akamua kumsamehe mmoja wapo , akamwambia:chaguwa mmoja wapo nimsamehe.
Huku akidhania kuwa atamchaguwa mwanawe.
Watu wote walitulia tuli,kimyaaa wakisubiri nani atamchaguwa,asamehewe.
Mwanamke Akanyamaza kitambo,kisha akasema: namchaguwa kaka yangu.
Hajaji akapigwa na butwaa na akamuliza :kwanini umemchagua kaka?
Akajibu:👇
💡AMA MUME YUPO (kwamaana anaweza kuja kuolewa na mume mwengine.
NA MTOTO ANAZALIWA (kwa maana atakapolewa tena anaweza kuzaa tena).
AMMA KAKA HAPATIKANI TENA(sababu baba na mama hawapo tena)
💡Maneno yake hayo👆 yakawa ndio mfano na hekima .
Na hajaji akapendezewa na hekima ya huyu dada.
Akamuwa kuwasamehe wote watatu.
🔦Muongozo:
Ndugu hakai katika nafasi yake yoyote mwengine..
Na wala hahisi thamani ya ndugu wa kike au kiume ila yule alieondokewa na mmoja wapo.
Hivyo basi:💡 hifadhi uhusiano baina yako na ndugu zako ..
kwa sababu ndugu ni kitu kisicholipika (nafasi yake haiwezi iziba mwengine)

ليست هناك تعليقات:

إرسال تعليق