الأحد، 26 مارس 2017

JE KUNA UKWELI GANI JUU YA HADITHI ISEMAYO

JE KUNA UKWELI GANI JUU YA HADITHI ISEMAYO MWENYE KUZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA INAADHINIWA BASI HATAWEZA KUTAMKA SHAHADA WAKATI WA KUTOLEWA ROHO.
______________________
KUNA MANENO HUEGEMEZWA KWA MTUME KUWA KASEMA :MWENYE KUZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA INAADHINIWA BASI HATAWEZA KUTAMKA SHAHADA WAKATI WA KUTOLEWA ROHO,
HAKIKA YA HADITHI HII HAINA UKWELI WOWOTE , WALA HAIJASWIHI KUEGEMEZWA KWA MTUME SWALALLA ALLAH ALAYHI WASALAM,
BALI NI MANENO YA UONGO YENYE KUZUSHIWA MTUME SWALALLA ALLAH ALAYHI WASALAM,
BALI MAZUNGUMZO WAKATI WA ADHANA INAADHINIWA AU KUZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA INAADHINIWA HILO NI JAMBO LENYE KUJUZU KISHERIA IKIWA KUNA HAJA YA KUZUNGUMZA,
BALI LILILOKUWA BORA NI KUNYAMAZA ILI KUPATA FURSA YA KUTEKELEZA SUNNA YA KURUDIA MANENO ANAYOYASEMA MUADHINI KAMA ALIVYOELEKEZA MTUME SWALALLA ALLAH ALAYHI WASALAM,
HII NDIO BORA KULIKO KUZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA, LAKINI SIO HARAM KUZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA,
WALA SIO KWELI KUWA UKIZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA INAADHINIWA BASI HUTAWEZA KUTAMKA SHAHADA WAKATI WA KUTOLEWA ROHO , HUU NI UONGO,
NA HAIFAI KUONDOA MUNKAR KWA KUTUMIA MUNKAR.
DALILI YA KUFAA KUZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA:
وقد روى مالك في الموطأ عن ابن شهاب عن ثعلبة بن أبي مالك القرظي:
انه أخبره :أنهم كانوا في زمان عمر بن الخطاب يصلون يوم الجمعة حتى يخرج عمر , فإذا خرج عمر وجلس على المنبر وأذن المؤذنون.قال ثعلبة : جلسنا نتحدث . فإذا سكت المؤذنون وقام عمر يخطب أنصتنا فلم يتكلم منا أحد . قال ابن شهاب : فخروج الإمام يقطع الكلام . ا
NA AMEPOKEA MAALIK KATIKA MUWATWA , KUTOKA KWA IBN SHIHAAB, KUTOKA KWA THAALABA BIN ABII MAALIK AL KURDHWIY:
KUWA ALIMPA HABARI: KWAMBA WAO WALIKUWA KATIKA WAKATI WA OMAR BIN AL KHATWAAB,
WALIKUWA WANASWALI SWALA YA IJUMAA,
MPAKA WAKATI ULE ANAPOTOKA OMAR KUPANDA KWENYE MIMBARI,
AKISHAPANDA OMAR KWENYE MIMBARI KISHA AKAKAA CHINI( ILI KUMPA FURSA MUADHINI AADHINI)
NA ANAADHINI MWENYE KUADHINI :
AKASEMA THAALABA:
BASI KITAMBO KILE MUADHINI ANAADHINI BASI SISI TUKAKAA HUKU TUNAZUNGUMZA:
NA AKISHAMALIZA MWENYE KUTOA ADHANA, KISHA OMAR ANAPOANZA KUKHUTUBU BASI SISI TWANYAMAZA (TWAKATA MAZUNGUMZO) NA HAKUNA YOYOTE ANAEZUNGUMZA,
AKASEMA IBN SHIHAAB:
BASI KITENDO CHA KUTOKA (KUPANDA)IMAM KWENYE MIMBARI KINAKATA MAZUNGUMZO,
.
فهؤلاء هم الصحابة رضي الله عنهم والتابعون في خير القرون يتكلمون في أثناء الأذان بمشهد من الخليفة الراشد المهدي عمر بن الخطاب رضي الله عنه. وهذا من الحجة الواضحة كل الوضوح على إباحة الكلام في أثناء الأذان,
HAO WALIKUWA NI MASWAHABA ALLAH AWARIDHIE PAMOJA NA MATABII KATIKA KARNE TUKUFU WALIKUWA WANAZUNGUMZA WAKATI KATIKATI YA ADHANA MBELE YA KHALIFA ALIYEONGOKA OMAR BIN AL KHATWAAB RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE,
NA HII NDIO HOJA YA WAZI KUWA INAFAA KUZUNGUMZA WAKATI WA ADHANA INAADHINIWA,
INGAWA LILILOKUWA BORA NI KUNYAMAZA ILI KUPATA SUNNA YA KUMUITIKIA MUADHINI ANAPOADHINI,
ZIYADA YA HAYO REJEA KWENYE
MUWATWA YA IMAM MAALIK.

ليست هناك تعليقات:

إرسال تعليق